“Changamkeni!” Tin alisema kwa sauti. “Hebu tusherehekee! Ama mnahitaji bendi la We Can Band iwasaidie?”
“Yebo, ndiyo!” umati ulijibu kwa sauti.
Tin aliangalia hapa na pale. “Bendi la We Can Band liko wapi? Ah hapana, siioni bendi hilo hapa. Tafrija haitafurahisha bila bendi. Nitahitaji usaidizi. Timu pekee ndiyo inayoweza kutimiza ndoto hii!” Tin alitabasamu huku akiangalia umati. “Kwanza, nitahitaji wapiga-ngoma wawili.”
Neo na Hope walikuwa wa kwanza kuweka mikono yao juu. Walipopanda kwenye jukwaa, Tin aliwapeleka kwa mikebe minne ya kahawa iliyo na vifuniko vya plastiki. Mikebe hiyo yalipambwa kwa karatasi inayong’aa na vitufe. Pia kulikuwa na mikwiro ya kutumiwa na Neo na Hope.
“Sasa tunahitaji mtikisaji,” Tin alisema.
“Josh! Mwite Josh!” Neo alisema kwa sauti.
“Kuna Josh kwenye umati huu? Josh yuko wapi? Hebu tumsaidie apande hapa jukwaani,” Tin alicheka.
Josh aliweka mkono wake juu. Wanaume wawili waliinua kiti chake cha magurudumu hadi jukwaani.
“Karibu, Josh,” Tin alisema. “Jaribu hawa watikisaji wawili.”
Josh alitikisa kifaa kimoja na kisha kutikisa kingine. Vifa hivyo vilitoa sauti tofauti.
“Hiyo ni vyema,” Tin alisema. “SASA, TAFRIJA…”
Lakini kabla aseme hayo, kulikuwa na sauti kubwa ya kengele. Kila mtu aliangalia hapa na pale kuona kilikuwa ni nini.
Kisha Noodle alikimbia jukwaani, akivuta mikebe iliyofungwa pamoja na uzi.
“Sauti za seti ya kengele!” Tin alisema kwa sauti. “Nilidhani nimepoteza.”
Bella alikimbia kuelekea jukwaani. “Noodle!” aliita. Noodle alikimbia kwenye Bella yuko, mikebe ikitoa sauti kubwa sana nyuma yake.
“Ni sawa,” Tin alisema akicheka. “Nafikiri Noodle anataka kuwa mmoja wa bendi la We Can Band. Na nafikiri anataka kujiunga nasi pia,” alisema akimnyoshea kidole Bella.
Tin alimsaidia Bella kupanda jukwaani na kusaidia kutoa mikebe ya kengele kutoka kwa mwili wa Noodle. Kisha Bella na Noodle walienda na kusimama karibu na Neo, Hope na Josh.
Tin alicheza gitaa yake na kusema, “HEBU TUCHEZE MUZIKI!”
Tin aliwanyoshea kidole Neo na Hope, walipiga ngoma zao. Kisha Tin akaimba, “Mguu wa kushoto nyuma,” na kunyooshea kidole umati.
“Mguu wa kushoto nyuma,” umati uliimba.
Kisha Tin akamnyooshea kidole Josh na akatikisa vitikisi vyake kuendana na mdundo wa muziki.
“Mguu wa kushoto kulia,” Tin aliimba.
“Mguu wa kushoto kulia,” umati uliimba.
Tin alimnyoshea kidole Bella. Mikebe iliyo kwenye laini ilitoa sauti nyororo wakati Bella aliiigonganisha. Noodle alitoa sauti ya furaha.
Punde si punde tafrija ilipendeza sana. Tin aliimba nyimbo zake huku Neo, Hope, Josh na Bella wakicheza naye. Na Noodle aliimba kwa sauti kila mara ili kushiriki pia!
Kisha kila mmoja wa wasanii wengine waliimba nyimbo kutoka nchi zao. Umati ulishangilia na kupiga makofi. Walipendezwa na burudani hiyo!
“Mmeona,” Tin alisema kwa bendi la We Can Band, “timu hii ndogo imetimiza ndoto! Asanteni kwenu nyinyi wanne … naNoodle, kila mtu alifurahia tafrija hiyo!”